Jinsi ya kujenga mafanikio ukiwa na mtaji wako


Na siku ya leo tutakwenda kujibu moja ya swali ambalo tumekuwa tukiulizwa sana na wasomaji wetu kwamba ni jinsi gani mtu anavyoweza kujijengea mafanikio ukiwa na mtaji wake.

Nasi kwa kuwa hatufungamani na upande wowote tutakwenda kujibu swali hili pasipo kuona aibu, hii kwa sababu moja ya kati ya kauli mbiu yetu inayotuongoza katika kufanya kazi, ni kuwafanya watu wote pasipo kuangalia dini wala kabila wawe na fikra sahihi kila wakati ili waweze kufanikiwa.

Na ukweli ni kwamba moja kati ya maswali ambayo watu wengi wanayo ni pamoja na hili, hii ni kwa sababu watu wengi huwa wanasema hawajafanikiwa kwa sababu hawana mtaji, lakini mara baada ya kupata mtaji utakuta watu haohao wanakosa katika mtaji huo wafanye kitu gani, swali linakuja hivi hujawahi kukutana na mtu akakwambia ya kwamba nina mtaji wa shilingi laki mbili lakini sijui nifanye kitu gani?

Bila shaka umewahi kukutana aina hii ya watu na kama hujawahi kukutana nao basi yawezekana ukawa ni wewe. Najaribu kujiohoji kwa sauti kubwa hivi hapa tatizo huwa linakuwa ni nini, mtu asipo fanikiwa atakwambia tatizo ni mtaji ila mara baada ya kupata mtaji atakwambia hajui afanye nini katika mtaji alionao.

Kwa muktadha huo hapa utagundua ya kwamba tatizo ni mawazo, narudia tena tatizo la watu wengi kutofanikiwa aidha kwa kuwa na mtaji au kwa kutokuwa na mtaji tatizo huwa ni mawazo chanya ni nini  mtu afanye ili aweze kufanikiwa.

Hivyo kitu cha msingi cha kuzingatia ili uweze kufanikiwa ukiwa na mataji wako ni kujua unataka nini katika maisha yako, hiki ndiyo kiwe kitu kikubwa cha kuzingatia kitakachokufanya wewe uweze kufanikiwa Zaidi.

Haijalishi ni kiasi gani ambacho kipo mkono mwako, kama lengo ni kuwa mfanyabiashara wa aina fulani ni vyema ukakaa chini na kutafakari kwa kina, tafakari kwa kina pasipo kuchoka. Na kutafakari huku kwa kina hakikisha anafanya uchanganuzi wa kutosha juu ya jambo unalitaka kulifanya.

Kwa mfano mkononi unayo laki tano kwa ajili ya mtaji fanya tathimini ya biashara ambayo unataka kuifanya, na tathimini hiyo hakikisha haimalizi mtaji wote kwa mara moja. Kama nilivyosema hapo awali kama una mtaji wa shilingi laki tano basi tathimini ya biashara yako iwe ni la shilingi laki nne. Kufanya hivi kutakusadia laki moja iliyobaki kuweza kutatua changamoto ndogondogo ambazo zitajitokeza katika biashara yako.

Hata hivyo katika biashara hiyo ambayo utakuwa umeanza kuifanya ni lazima uwe na daftari la mahesabu ya biashara yako, daftari hili utaandika mapato na matumizi katika biashara yako, kufanya hivi itakusaiadia kujua kama unapata faida au laah. Pia mali bila daftari hupoteaa bila habari.

Lakini jambo jingine katika mtaji ulionao hakikisha unaulinda kwa nguvu zote kama mboni ya jicho lako, kufanya hivi kutakutoa wewe katika orodha ya watu ambao huanzisha miradi au biashara kisha biashara hizo kufa.