Madaktari wa China watibu watu milioni 220 Afrika


Kwa miaka 56 sasa, China imekuwa ikituma madaktari wake kutoa huduma za matibabu katika bara la Afrika. Kwa ujumla, taifa hilo la Asia limetuma madaktari 21,000 barani Afrika na kuweza kutibu jumla ya watu milioni 220.

Lin Xiaojun anatoka kwa moja ya familia za Wachina ambazo zimekuwa barani Afrika kwa vizazi vitatu zikitoa msaada wa matibabu.

“Kufanya kazi hapa Zanzibar kama daktari ni kitu cha kawaida katika familia yetu,” Lin ambaye aliwasili Zanzibar mwezi Julai alisema.

Ameendelea kwa kusema “Mnamo mwaka wa 1997, mama mkwe wangu Zhou Xiaoyu alikuwa hapa Zanzibar kwa muda wa miaka miwili katika operesheni ya kutoa msaada wa matibabu, mjomba wake Zhou Zhiyao naye alikuja hapa mwaka wa 1964 na 1977 pamoja na madaktari wa kutoka China,” alisema Lin.


Mpya zaidi Nzee zaidi