Mahakama Kuu ya Tanzania yamuitwa Tundu Lissu


Mahakama Kuu ya Tanzania imetoa hati ya wito wa kufika mahakamani kwa mbunge wa zamani Singida Mashariki, Tundu Lissu kwa ajili ya shauri la maombi yake kuanza kutajwa.

Wito huo kwa Lissu umetolewa leo na kusainiwa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania kufuatia Lssu kufungua maombi mahakamani hapo chini ya hati ya dharura, kupitia kwa kaka yake Alute Mughwai ambaye amempa mamlaka ya kisheria kufanya hivyo.

Katika maombi hayo namba 18 ya mwaka 2019, Lissu anaomba kibali cha kufungua shauri dhidi ya Spika wa Bunge la Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania, kupinga kuvuliwa ubunge wake.

Ikumbukwe uamuzi wa kumvua ubunge ulitangazwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai Juni 28 mwaka huu wakati akiahirisha mkutano wa 15 wa Bunge.