Loading...

8/12/2019

Mashabiki wamkataa Neymar PSG

Mashabiki wa Paris Saint-Germain wamemtolea uvivu mshambuliaji Neymar katika mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu Ufaransa iliyochezwa jana.

Licha ya kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Nimes, mashabiki wa PSG walikwenda uwanjani na mabango ya kumtaka Neymar kuondoka ndani ya klabu hiyo.

Neymar ameibua mzozo wa muda mrefu na klabu yake akishinikiza kuondoka katika usajili wa majira ya kiangazi.

Miamba ya soka Hispania Barcelona na Real Madrid, inahusishwa na mpango wa kumsajili nahodha huyo wa zamani wa Brazil.

Mbali na kwenda mabango, mashabiki hao walipaza sauti wakitaka PSG kuharakisha uhamisho wa Neymar kwa kuwa hawamtaki.

Mashabiki wa PSG hawaoni mchango wa Neymar kama Kylian Mbappe, Edinson Cavani na Angel Di Maria ambao wamekuwa wafungaji wa timu hiyo katika mechi za mashindano.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger