Meli ya mafuta ya Iran ambayo imesababisha mvutano kati ya Marekani na Iran imebadili mkondo na sasa inaelekea Uturuki badala ya kusini mwa Ugiriki.
Meli hiyo ya "Adrian Darya 1" ambayo zamani ilikuwa ikiitwa Grace 1, iliachiwa kutoka kizuizini Gilbraltar katikati ya mwezi huu baada ya mkwamo wa wiki tano kutokana na madai kwamba ilikuwa inapeleka mafuta ya Iran nchini Syria hatua inayokiuka vikwazo vya Umoja wa Ulaya.
Taarifa za awali zilionesha kuwa meli hiyo ambayo imebeba mafuta, ilikuwa ikielekea katika bandari ya Kalamata kusini mwa Ugiriki.
Lakini takwimu zilizotolewa leo na Idara ya Usafiri wa Majini, zinaonesha kuwa meli hiyo sasa inaelekea Uturuki kupitia Bahari ya Mediterania na itatia nanga katika bandari ya Mersin Agosti 31.
Marekani ambayo inasema meli hiyo inamilikiwa na kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Iran, ambacho Marekani imekiorodhesha kama kundi la kigaidi, imezitaka nchi katika ukanda huo kutoisaidia.