Ombaomba kulipia vibali ili waweze kuomba mitaani

Huko nchini Uswizi katika mji wa Eskilstun imepitishwa sheria inayowataka ombaomba watahitajika kulipia Euro kulipia Euro 21 ili waweze kupewa kibali cha kuomba mitaani.

Kwa mujibu wa gazeti la the Guardian, wale wote watakaohitaji kuomba katika mitaa ya mji wa Eskilstun watahitajika kuomba ruhusa ya kufanya shughuli hiyo kwa miezi 3. Atakaye kutwa anaomba bila kuwa na ruhusa hizo atatozwa faini ya Euro 342.

Ombaomba wote watahitajika kuomba kupita Intanet au kituo cha polisi makaratasi ya vibali vya kuwaruhusu kufanya shughuli hiyo ya kuomba mitaani. Sheria hiyo mpya imeanza kutumika mwanzoni mwa mwezi.

Kwa mujibu wa runinga ya taifa ya Uswizi, SVT tangu kuanza kutumika kwa sheria hiyo mpaka hivi sasa ni watu 8 ambao wamekwisha patiwa vibali.