Polisi Dar es Salaam wadaiwa kumzuia Mshauri Mkuu wa ACT Wazalendo, Ndugu Maalim Seif Sharif Hamad akiwa tayari amewasili ofisi za ACT Temeke kwaajili ya kufungua matawi mapya ya chama hicho Temeke, Dar Tanzania.
Polisi wamewakamata viongozi wa ACT wakiwemo baadhi wa Mkoa wa Dar es salaam pamoja na Katibu wa Kamati ya Uadilifu Taifa, Ndugu Mbarara Maharagande na kupelekwa kituo cha Polisi cha Chang'ombe.
Lakini pia Polisi wamewakamata baadhi ya waandishi wa Habari na kujumuishwa kwenye kamata kamata hiyo,
