Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amefanya mazungumzo na waziri wa Mambo ya Kigeni wa Iran, Mohammad Javad Zarif kabla ya mkutano wa nchi saba tajiri duniani - G7, ambako atajaribu kuituliza mivutano kati ya Iran na Marekani katika kile kinachotishia kuwa mkutano mkali wa kilele.
Akizungumza leo baada ya kukutana na Zarif katika Kasri la Elysee, Macron amesema hali imefikia katika hatua ngumu, kutokana na mpango wa Iran kutaka kujiondoa katika mkataba wa kimataifa wa nyuklia uliofikiwa na madola yenye nguvu ili kuidhibiti mipango ya nyuklia ya Iran.
Ufaransa imeimarisha juhudi za kumshawishi Rais wa Iran, Hassan Rouhani, huku Macron akimtuma mara mbili mshauri wake wa kidiplomasia Emmanuel Bonne mjini Tehran katika miezi ya hivi karibuni.