Klabu ya Inter Milan imethibitisha kusajili mshambuliaji Romelu Lukaku kutoka klabu ya Manchester United kwa mkataba wa miaka mitano kwa ada ya £73m.
Lukaku aliwasili Italia kwaajili ya vipimo vya afya siku ya Jumatano na sasa amekamilisha usajili huo utakaomfanya awepo San Siro hadi Juni 30 2024.