Salma Kikwete awaasa wananchi wanufaike na elimu wanayopata kwenye viwanja vya maonesho

Mbunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Salma Kikwete amewaasa wananchi wanaotembelea na kuhudhuria maonesho, yakiwamo ya wakulima(Nanenane) watumie elimu wanayopata katika maonesho hayo kuboresha uchumi wao.

Salma ambaye ni mke wa Rais mstahafu wa awamu ya nne wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania( mheshimiwa Jakaya Kikwete) ametoa wito huo katika kilele cha maonesho ya wakulima( Nanenane) kanda ya Kusini katika viwanja vya Ngongo, manispaa ya Lindi.

 Alisema maonesho, hasa ya wakulima yanaweza kuwa na tija iwapo wataamua kutumia kikamilifu elimu wanayopata kupitia maonesho hayo.

Alisema wananchi wanauwezo wa kujenga na kuinua uchumi wa kaya zao wilaya, mikoa na taifa, iwapo watakwenda  nyumbani kwao na maarifa wanayopata kutoka kwenye viwanja vya maonesho.

 '' Tumieni maonesho ya nanenane kujifunza, badala ya kuyaacha kwenye mabanda ya maonesho,'' alisema mbunge Kikwete.

Mbali na hayo, alirejea kutoa wito ambao amekuwa akito  a mara kwa mara. Aliwaomba na wazazi na walezi wawahimize watoto wakike wapende na kwenda shule.

Huku akisisitiza walezi na walezi hao wahakikishe watoto wanatimiza ndoto zao za mafanikio kielimu na maisha.

Alisema miongoni mwasababu zinazochangia kukatiza ndoto za watoto hao wakike ni mimba za utotoni.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items