Loading...

8/13/2019

Viingilio kuziona Simba SC na Azam FC katika Ngao ya Jamii


Mchezo wa Ngao ya Jamii kuashiria kuanza kwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara (TPL) utafanyika Jumamosi wiki hii  Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. Mchezo huo utawakutanisha mabingwa wa Ligi Kuu, Simba SC dhidi ya washindi wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Azam FC.

Taarifa ya TFF imesema kwamba viingilio katika mchezo huo vitakuwa vya madaraja mawili tu, Sh 5,000 kwa majukwaa ya mzunguko na Sh. 10,000 kwa maeneo ya VIP B na C.

Simba SC ndio mabingwa wa Ngao ya Jamii msimu uliopita baada ya kuichapa Mtibwa Sugar 2-1 Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza Agosti 18, mwaka jana.

KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger