Wakusanya Damu kwa ajili ya Majeruhi wa ajali ya Moto Morogoro


Benki ya Exim Tanzania kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS) kesho Agosti 14 wanatarajia kuendesha zoezi la uchangiaji damu kwa ajili ya kuwasaidia majeruhi wa ajali ya moto iliyosababishwa na lori la mafuta lililopinduka na kulipuka eneo la Msamvu Mkoani Morogoro ambapo watu zaidi ya 70 walifariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Zoezi hilo linalotarajiwa kufanyiika katika viwanja vya kituo cha mabasi cha Mbagala, Wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, kuanza majira ya saa 2:00 asubuhi hadi saa 11:00 jioni jioni.

Mkuu wa idara ya masoko na mawasiliano wa benki hiyo, Stanley Kafu ametoa wito kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam na mikoa jirani kujitokeza kwa wingi kwenye viwanja hivyo ili kushiriki katika zoezi hilo muhimu.