https://monetag.com/?ref_id=TTIb wajawazito watakiwa kuhudhuria kliniki Songwe Inbox x | Muungwana BLOG

wajawazito watakiwa kuhudhuria kliniki Songwe Inbox x

Na, Baraka Messa, Songwe.

PAMOJA na Serikali kujenga vituo mbalimbali vya afya nchini kwa lengo la kutatua chganga moto za afya hasa kwa mama na mtoto Mkoani Songwe bado kuna changamoto ya akina mama wajawazito  kutohudhuria kliniki katika vituo vya afya na kujifungulia majumbani na kwa wakunga wa jadi, jambo ambalo huhatarisha afya ya mama na mtoto pindi anapojifungua.

Daktari Bingwa Magonjwa ya Wanawake na Afya ya Uzazi Hospitali ya Mkoa wa Songwe Dokta Lukombodzo Lulandala akiongea na mwandishi wa gazeti hili  alisema kuwa mpaka hivi sasa katika mkoa wa Songwe takwimu zinaonyesha kuwa  bado kuna akina mama wanajifungua njiani na wengine nyumbani hali ambayo huhatarisha maisha ya mama na mtoto .

alisema takwimu za mwaka 2018 zinaonyesha kuwa kunachangamoto ambazo inatakiwa jamii ibadilike hasa vijijini ili kupunguza na kukomesha kabisa tabia ya baadhi ya akina mama kutohudhuria hospitalini na kujifungua majumbani.

" kwa mwaka jana 2018 imeonyesha  akina mama waliojifungua katika vituo vya kutolea huduma kwa mwaka inafika  36,660 (79%), waliojifungulia njiani kuelekea vituo vya afya ni wapatao 1505 (3%)  waliojifungulia  kwa wakunga wa jadi ni 222 (0.4%) na waliojifungulia nyumbani ni wapatao 1193(2.6%), bado tuna kazi kubwa kuhakikisha  akina mama wote wajawazito wanajifungulia katika vituo vya kutolea huduma" alisema Dk Lulandala.