Kimbunga Lekima kikiandamana na mvua kubwa na upepo mkali mepama leo kimelipiga eneo la pwani ya kusini-mashariki wa China.
Zaidi ya watu 700, waliokolewa katika maeneo hayo kabla ya kuwasili kimbunga hicho, ambacho kinatarajiwa kusababisha mvua kubwa katika miji ya Hangzhou na Shanghai.
Katika mji wa Shanghai, vivutio vingi vya utalii vimefungwa, makumbusho na hifadhi za wanyama kadhalika vimefungwa. Safari nyingi za mwendo kasi za reli pamoja na za ndege 100 zimesitishwa.
Kimbuga hicho ambacho hadi sasa kinaelezwa kusababisha vifo vya watu 13, awali kimeyapiga mataifa ya Japan na Taiwan.