Adaiwa kumuua mkewe na kumtupa migombani, Polisi wamtia nguvuni


Jeshi la Polisi Mkoani Arusha linamshikilia Amir Hassan kwa tuhuma za  kumuua mke wake, Lidya Kiwale usiku wa kuamkia leo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Jonathan Shana amesema tukio hilo limetokea kijiji cha Majengo  na baada ya mauaji hayo Hassan anatuhumiwa kutupa mwili kwenye migomba jirani na makazi yake.

"Tumepata taarifa za tukio hili ambalo limetokea usiku wa kuamkia leo (Jumapili) na mtuhumiwa tayari ameshikiliwa na polisi kwa mahojiano, “amesema.

Ikumbukwe tukio hili ni mfululizo wa matukio ya wanawake kuuawa kikatili katika mji wa Mto wa mbu ambayo yamedumu kwa zaidi ya miaka mitatu ambapo wanawake 11 wameuawa hadi kufikia sasa.