Malindi SC yachapwa goli 4-1 na Al Masry kombe la Shirikisho Afrika


 Na Thabit Madai-Zanzibar

Mchezo wa kwanza Roundi ya Pili  Kombe la Shirikisho barani Afrika kati ya Timu ya Malindi SC dhidi ya timu ya Al Masry ya Nchini Misri umemalizika kwa timu ya Malindi SC  kushindwa kutamba katika uwanja wa nyumbani kwa kufungwa goli 4-1.

Mchezo huo wa kukata na shoka ulipigwa katika Dimba la Amani Stadium majira ya Saa 10:00 za jioni

Magoli katika Mchezo huo yalifungwa na Mahmoud Wadi dakika ya 27, Hassani Ibrahimu dakika ya 32, Mahmoud ally dakika ya 39, na Seido Simpore dakika 52 goli pekee la Malindi lilifungwa dakika ya 42 na Ibrahimu Abdalla.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kumaliza kwa Mchezo huo, Kocha wa Timu ya Malindi SC, Saleh Ahmed Machupa amesema mchezo kwao ulikuwa mgumu japokuwa walitengeneza nafasi nyingi ila walishindwa kuzitumia ambapo wapinzani wao walipata na kuzitumia na kuibuka na ushindi huo.

Nae Nahondha wa Timu ya Malindi SC alisema kuwa mchezo ulikuwa mgumu kwao kutokana wachezaji wengi walikuwa katika kikosi chao hawana uzoefu na mashindano ya kimataifa. Aliongeza kusema kuwa haya ni matokeo wanatakiwa kuyakubali na kikubwa  kujipanga na michezo unaofuata.

Naye Menaja wa Timu ya Al Masry, Yasr Salim alisema kuwa wamepokea vizuri matokeo hayo kwani waliyatarajia kuyapata kutokana na wachezaji waliokuwa nao.