Bomu la kutegwa laua watu sita Somalia

Afisa mmoja nchini Somalia amesema wanasiasa wawili, walinzi watatu na mfanyakazi mmoja wa misaada ya kiutu wameuwawa kufuatia shambulio la bomu lililotegwa barabarani mjini Mogadishu.

 Mohamed Abdi Waare rais wa nchi hiyo amesema katika taarifa yake kwamba shambulio hilo lilitokea katika njia panda kati ya mji wa Bal'ad na Jowhar katika jimbo la Hirshabelle kilomita 100 kaskazini mwa mji mkuu Mogadishu.

Kundi la kigaidi la Al Shabaab limekiri kuhusika na shambulio hilo. Kundi hilo linalofungamanishwa na mtandao mkubwa wa kigaidi wa al Qaeda linafanya mashambulio ya mara kwa mara katika taifa hilo dhaifu Mashariki mwa Afrika.