Choo cha dhahabu chenye thamani ya Dola Milioni 1.25 chaibwa


Polisi katika mji wa London, nchini Uingereza wanatafuta choo cha dhahabu chenye thamani ya dola milioni 1.25 ambacho kiliibwa kutoka kwenye ikulu ya Blenheim Palace.

Choo hicho kiliwekwa kama mapambo ya ikulu ya Blenheim alikozaliwa waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Winston Churchil.

Wizi huo uligunduliwa siku mbili tu baada ya choo hicho kuwekwa kwenye ikulu hiyo. Waliotembelea ikulu ya Blenheim waliruhusiwa kutumia choo hicho ilimradi wamalize haja yao chini ya muda wa dakika tatu.