Dodoma FC na Gwambina FC hakuna mbabe


Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.

Timu za Dodoma FC na Gwambina FC ya Misungwi, jijini Mwanza wameshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya kufungana bao moja kwa moja katika mchezo wa kirafiki uliochezwa Jana jumamosi kwenye uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Katika mchezo mkali na wakusisimua kutokana na timu zote kucheza kiufundi na kukamiana sana, ilishuhudiwa hadi kipindi cha kwanza kina malizika timu hizo zilikuwa suluhu ya kila timu haikuweza kupata bao.

Gwambina ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na mkongwe Jokobo Masawe, baada ya kumalizia mpira uliotemwa na kipa wa Dodoma FC Emanuel Mseja na kufanya Gwambina kuongoza kwa bao moja bila.

Dodoma FC walisawazisha dakika za mwisho  kwa mkwaju wa penati, baada ya mchezaji wa Gwambina kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari, na mkwaju huo wa penati kufungwa na Hamadi Kibopile.

Mchezo huo ulikuwa ni wanne wa kirafiki kwa Dodoma FC na michezo yote imetoka sare, Gwambina leo jumapili watashuka tena kwenye uwanja huo huo kucheza na Fountain Gate inayoshiriki ligi daraja la pili Tanzania bara.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia