https://monetag.com/?ref_id=TTIb Mchezaji wa Manchester United aondolewa kwenye kikosi cha Uingereza | Muungwana BLOG

Mchezaji wa Manchester United aondolewa kwenye kikosi cha Uingereza

Kiungo wa klabu ya Manchester United Jesse Lingard ameondolea kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Uingereza na kurudi kwenye klabu yake kwasababu za kuumwa.

Lingard 26 hakuweza kushiriki mazoezi ya Ijumaa na kikosi hicho cha Uingereza kilichokuwa kikijiandaa na mchezo wa kufuzu mashindano ya Euro 2020 dhidi ya Bulgaria kwenye dimba la  Wembley leo Jumamosi na mchezo mwingine utakaopigwa kwenye dimba la St Mary dhidi ya Kosovo Jumanne.