Rais wa Barcelona afunguka kuhusu Neymar

Barcelona haitamsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar mwezi Januari, kulingana na rais wa mabingwa hao wa Uhispania Josep Maria Bartomeu.

Mabingwa hao wa La Liga walijaribu msimu wote huu kuzungumza kuhusu mkataba wa kumsaini kiungo huyo wa Brazil ambaye alihamia Ufaransa kwa dau lililovunja rekodi la £200m mwaka 2017.

Hatahivyo klabu hizo mbili hazikukubaliana.

Alipoulizwa iwapo kulikuwa na uwezekano wa Barcelona kumsaini Neymar mwezi Januari , Bartomeu alisema kwa sasa hapana.

Neymar alikuwa mchezaji ghali zaidi 2017 wakati PSG ilipolipa Yuro Milioni 222 ili kuweza kuondoka Barcelona.

Mshambuliaji huyo amefunga magoli 34 katika misimu miwili akiichezea miamba hiyo ya Ufaransa, ijapokuwa majeraha yaliathiri kampeni yake katika misimu yote miwili.

Bartomeu alipinga mapendekezo hayo kwamba klabu hiyo ilikuwa ikimlenga sana Neymar msimu huu akiongezea kwamba uwezekano wa kumsaini lilikuwa swala la ziada tu.

Akizungumza katika mtandao rasmi wa runinga ya klabu hiyo aliongezea: Barca tayari imepanga kikosi chake. Fursa ya kumsaini Neymar ni mojawapo iliojitokeza katika soko. Usajili wake ungekuwa wa ziada, haukupangwa.