Natamani Watendaji wa Uganda waje Tanzania angalau mwezi mmoja tu - Rais Magufuli


Rais wa Tanzania,  Dk. John Pombe Magufuli amemtaka Rais wa Uganda, Yoweri Museveni wa Uganda kuwa mkali kwa watendaji, ili kuhakikisha mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima Uganda mpaka Tanga, unatekelezwa kwa wakati, tofauti na sasa ambapo unasuasua.

Aliyasema hayo wakati akifungua kongamano la biashara kati ya Tanzania na Uganda, jijini Dar es Salaam, ambapo yeye na Museveni walikuwa wageni rasmi.

Kutokana na hilo, amesema anatamani watendaji wa Tanzania wangeenda Uganda na wa Uganda waje Tanzania ili ashughulike nao angalau kwa mwezi mmoja tu.

 “Nilikuwa namwuliza mzee Museveni mbona unachelewesha hili bomba, kwa sababu ya kodi ya huko ambayo umekataa kuikubali ya dola 600 wakati utakuwa unatengeneza dola bilioni 800, jitolee hii kodi kidogo utengeneze ajira na utakuwa unapata fedha.

“Kwa muda mrefu watu wako wa URA yaani Uganda Revenue Authority wamekuwa wakikuchelewesha, sisi tulitaka hilo bomba liitwe Kaguta Pipeline siku tunapozindua, hao wasikucheleweshe.

“Nikamtolea mfano Museveni kuwa nilipoingia madarakani tayari nimebadilisha makamshina watano wa TRA, si suala la kujidai ni baya, lakini nikamwambia wewe umemg’ang’ania wa nini huko? Tunatakiwa tusonge mbele kibiashara.

“Imebidi tulizungumze hili maana mimi linaniuma, tulibidi tupeleke mabadiliko ya sheria ya kodi ili hili bomba lijengwe, sisi Tanzania mikoa minane itafaidika na hili bomba likishaanza collection ya revenue (makusanyo ya kodi) ya Uganda itakuwa ndiyo inaongoza katika uchumi wa bara la Afrika sasa kwanini ucheleweshwe na watendaji?

“I wish (ninatamani) hawa watendaji wa Tanzania wangeenda Uganda na wa Uganda waje Tanzania ili ni-deal (nishughulike) nao angalau kwa mwezi mmoja tu,” alisema Rais Magufuli.

Magufuli aliwataka watendaji katika nchi za Uganda na Tanzania wahakikishe wanafanikisha miradi mikubwa ambayo inatengeneza ajira nyingi.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia