Diwani anusa Ufisadi TARURA



Diwani, Deogratius Ndega wa Kata ya Bumera Halmashauri ya Tarime vijijini mkoani Mara kupitia Chama cha mapinduzi CCM amesema kuwa ameokoa shilingi Milioni 24 na laki 5 zilizokuwa zimetengwa na wakala wa Barabara TARURA  ili kufanyia matengenezo barabara ya Kwisarara,Taisi,Matamankwe,Turugeti yenye urefu wa kilomita 8 wakati ilishafanyiwa matengenezo hayo hapo nyuma.

"Ndugu mwenyekiti wa Baraza la madiwani halmashauri ya Tarime Vijijini Mimi binafsi nasema katika baraza lako tukufu kuwa nimeokoa shilingi minilioni 24 laki 5 zilizokuwa zimetengwa na wakala wa Barabara TARURA kwa ajili ya matengenezo ya Barabara ya Kwisarara, Taisi, Matamankwe, Turugeti iliyokuwa imetengewa fedha shilingi milioni 24.5 kwa mwaka wa fedha 2018/2019 mimi nasema kuwa barabara hiyo ilikwisha fanyiwa matengenezo hapo nyuma kwa hali hiyo fedha  ilikuwa iingine mifukoni mwa watu,"alisema Ndege.

Ndege aliongeza kuwa Barabara ya kwisarara,Taisi,Matamankwe,Turugeti yenye juma ya kilomita 11 ilitengewa fedha ya matengenezo kwenye bajeti ya mwaka 2016/2017 na ilifanyiwa matengenezo hayo leo hii nashangaa kuona barabara hiyo hiyo ikibadilishwa jina na kuitwa Kwisarara,Matamankwe,Turugeti yenye urefu wa kilomita 30 na kuombewa fedha tena ya matengenezo shilingi milioni 30 kitu ambacho nibatili.

Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya Tarime vijijini,Yomami Misiwa alisema kuwa kwenye halmashauri yake hapendezewi kuona mambo kama hayo yakitokea kwani yanaweza kuisababishia halmashauri yake kupata hati chafu.

Misiwa aliwataka watu wa TARURA kuja katika Baraza hilo kwenye kikao kingine kijacho ili kutoa taarifa mbele ya madiwani kwani kufanya hivyo majibu hayo yatawaondolea madiwani dukuduku kuwa fedha za serikali zainazotolewa kwa ajili ya wananchi zinawafikia walengwa.

Kwa upande wake Fundisanifu wa halmashauri ya Tarime Vijijini,Nancy Kahupale aliliambia baraza hilo kuwa hana majibu ya moja kwa moja ila anachokijua ni kuwa walaka wa Barabara TARURA wanaidai halmashauri ya Tarime Vijijini zaidi ya shilingi milioni 100.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia