Wale wa ‘nitumie kwenye namba hii’, Bunge lawatungia sheria kuwabana


Bunge limepitisha Marekebisho ya Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta Sura ya 306, ambao utawabana wanaotumia simu kufanya utapeli.

Sheria hiyo ni miongoni mwa sheria saba zilizowasilishwa Bungeni na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Prof Adelardus Kilangi, kupitia Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Namba Tano wa mwaka 2019.

Akiwasilisha mudwada huo, Kilangi alisema sheria hiyo iliyotungwa na Bunge mwaka 2010 ililenga kushughulikia masuala ya mawasiliano ya kielektroniki, kuweka mfumo wa kudhibiti na kusimamia watoa huduma katika sekta ya mawasiliano ya kielektroniki na posta.

 “Marekebisho yanayopendekezwa yanalenga kuimarisha udhibiti wa matumizi ya huduma za mawasiliano ya kielektroniki, kudhibiti watumiaji wa mawasiliano wenye lengo la kurubuni watu kwa kutumia laini za simu zilizosajiliwa kwa majina tofauti na majina yao halisi.

“Pia umenuia kuimarisha usalama wa watumiaji wa huduma za kimtandao na kupunguza wimbi la uhalifu na kuhuisha sheria hii ili iendane na hali ya sasa ya usajili wa laini za simu kwa alama za vidole,” alisema.

Kwa upande wa muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Baraza la Taifa la Mitihani Sura ya 107, mabadilio yanayohusu kupanua wigo wa baraza hilo kwenye upimaji wa wanafunzi na kuongeza aina mpya ya makosa na adhabu zitakazotolewa kutokana na ukiukwaji wa taratibu za mitihani.

Prof. Kilangi alisema kifungu cha pili cha sheria hiyo iliyotungwa na Bunge mwaka 1973 kinarekebishwa kwa madhumuni ya kufafanua baadhi ya maneno na misamiati inayotumika chini ya sheria hiyo.


Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia