Rorya watangaziwa kanuni za uchaguzi wa Serikali za mitaa


Na. Timothy Itembe Mara

Msimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa wilaya Rorya mkoani Mara,Gabriel Njige amesema kuwa anatarajia kuona uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika hapo 24,11,2019 kuwa wa huru,haki na Amani tofauti na chaguzi zilizopita.

Kauli hiyo ameitoa jana kwenye kikao kilichowashirikisha viongozi ngazi ya Vitongoji na Vijiji na kata kwa maana ya watendaji ambao walikalia katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya Rorya.

Njige alisema kuwa lengo la kikao hicho kuwakutanisha ni kwa ajili ya kupokea Tangazo la  majina na mipaka ya vijiji na vitongoji kwa maandalizi ya uchaguzi wa Mwenyekiti wa kijiji wajumbe wa halmashauri ya kijiji na Mwenyekiti wa kitongoji unaotarajia kufanyika Nxchi znima na halmashauri ya wilaya Rorya ikiwemo.

"Msimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa katika halmashauri ya Rorya kwa mamlaka aliyopewa chini ya kanuni ya 5 ya kanuni za uchaguzi wa Mwenyekiti wa kijiji wajumbe wa halmashauri ya kijiji na Mwenyekiti wa kitongoji,tangazo la serikali namba 373 la tarehe 26/04/2019 pamoja na kanuni za uchaguzi wa Mwenyekiti wa kitongoji  katika mamlaka za miji  midogo,Tangazo la serikali namba 371la tarehe 26/04/2019 na kwa kuzingatia orodha ya vijiji na vitongoji vilivyotangazwa katika Gazeti la serikali namba 537 la tarehe 19/7/2019 anatangaza majina na mipaka ya vijiji na vitongoji kwaajili ya uchaguzi wa mwenyekiti wa kijiji,wajumbe wa halmashauri ya kijiji na mwenyekiti wa kitongoji katika halmashauri ya Rorya,"alisema Njige.

Mkuu wa wilaya Rorya,Saimon Chacha aliwataka wanajamii pamoja na wawasimamizi wa uchaguzi kuzingatia sheria na kanuni pamoja na taratibu  zilizopo kwani zoezi ni la kikatiba.

Kwa upande wake Askofu wa kanisa la Menonite Tanzania Rwanga Katite alipongeza Rais awamu ya Tano,John Pombe Magufuli kwa maandalizi mazuri yaliyopo ili kufikia uchaguzi wa serikali za mitaa.

Katite alisema kuwa katika uchaguzi uliombele yetu wapiga kura wasiwe na wasiwasi kwani haiwahi kutokea katika chaguzi zote zilizopita kuwa na maandalizi mazuri kama uchaguzi huu wa awamu ya Tano.

Naye Ayoub Murimi alimaliza kwa kutaja jumla ya vjiji 87 na vitongoji 508 majina na mipaka ya vijiji na vitongoji vilivyopo katika halmashauri ya wilaya Rorya.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items