https://monetag.com/?ref_id=TTIb Serikali yaja na mbinu mpya kuwabaini wanufaika hewa TASAF | Muungwana BLOG

Serikali yaja na mbinu mpya kuwabaini wanufaika hewa TASAF


Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma

Serikali imesema imejipanga kuhakikisha inaboresha mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF kwa kuanza kutoa huduma hiyo kielectronic sambamba na kuwaondoa wanufaika ambao hawana sifa za kunufaika na mpango guo.

Hayo yamebainishwa na Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya utumishi wa Umma na utawala Bora, Mary Mwanjelwa, alipokuwa akijibu swala mbunge Eng. Ramo Makani(Tunduru Kaskazini) aliyehoji lini serikali itachukua hatua za maksudi kurekebisha kasoro za baadhi ya wanufaika wa mpango huo ambao hawasitahili.

Dkt Merry amesema serikali imekuwa ikifanya jitihada za maksudi kuhakikisha mpango wa TASAF unawanufaisha wahusika pekee yao kwa kuanza kutoa huduma hiyo kwa njia ya kielectronic na kuwaondoa wasiostahili kunufaika na mpango wa kunusuru kaya masikini.

Amesema mfumo huo itasaidia kuwatambua wanufaika ambao hawakutakiwa kuwepo kwenye mpango huo na watawaondoa katika mfumo huo haraka.

Aidha amesema baadhi ya changamoto ambazo mpango unakabiliana nazo ni kilio kutoka kwa baadhi ya wananchi masikini ambao hawajafikiwa na huduma ya mpango huo kwenye vijiji/ Mitaa/shehia takribani 5,693 ambavyo havikufikiwa katika awamu ya kwanza ya mpango huo.

Malalamiko mengine ni walengwa kuhusu Makato ya fedha kipindi cha malipo na kusema swala hilo walengwa wanaendelea kuelimishwa kwanini Makati yanatokea, amesema hayo yanatokea ni kutokana ni kutimiza masharti ya kupikwa ruzuku hasa kwa kaya zenye watoto walio shuleni na wale wanaotakiwa kuhudhuria kliniki ambao ni watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

Akibainisha kuwa endapo kaya itashindwa kutimiza masharti watoto kuhudhuria shuleni au kutokupeleka watoto kliniki fedha hizo zitakatwa Kama adbabu na kuomba wabunge waendelee kutoa elimu kwa wananchi majimboni mwao.