Wabunge wa Uingereza wameupinga mswada wa Waziri Mkuu Boris Johnson juu ya kuitisha uchaguzi wa mapema. Johnson alitaka uchaguzi huo ufanyike kabla ya Uingereza kujiondoa Umoja wa Ulaya tarehe 31 mwezi Oktoba.
Ni wabunge 293 tu walioumuunga mkono Johnson. Idadi hiyo haikufikia thuluthi 2 zilizohitajika katika bunge lenye jumla ya wajumbe 650.
Wabunge wa upinzani walipiga kura kupinga na wengine hawakushiriki katika kupiga kura. Mpango wa Waziri Mkuu Johnson ni kuitisha uchaguzi huo, wiki mbili kabla ya siku ya Uingereza kutoka kwenye Umoja wa Ulaya lakini wabunge wa vyama vya upinzani wamesema hawataunga mkono kufanyika uchaguzi kabla ya Waziri Mkuu kwenda Brussels, kuomba Uingereza iongezewe muda wa Brexit ili kuhakikisha kwamba haiondoki Umoja wa Ulaya bila ya mkataba.
Hata hivyo Waziri Mkuu huyo amepania kupinga kuomba muda zaidi. Wakati huo huo serikali imesimamisha rasmi shughuli za bunge kwa muda wa wiki tano wakati mgogoro wa Brexit bado unaendelea.
Wabunge watarejea takriban wiki mbili kabla ya tarehe 31 Oktoba, siku ambapo Uingereza inapaswa kuondoka Umoja wa Ulaya.