Watatu wauawa kwenye shambulizi la bomu kusini mwa Somalia


Watu watatu wameuawa ikiwa ni pamoja na ofisa wa serikali ya mtaa katika shambulizi la bomu lililotegwa barabarani kwenye barabara inayounganisha miji Bal'ad na Jowhar katika jimbo la Shabelle ya kati.

Msemaji wa jimbo hilo Bw. Da'ud Haji Irro amesema bomu hilo lililotegwa katika kijiji cha Gololey lililipuka wakati maofisa serikali wanapita katika jimbo hilo. Kundi la Al-Shabaab limetangaza kuwajibika na shambulizi hilo.

Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM imetoa mwito kwa vikosi vyake kuimarisha mapambano dhidi ya kundi la Al-Shabaab ili kulinda usalama wa barabara, na kuwezasha usafirishaji wa watu na bidhaa.