https://monetag.com/?ref_id=TTIb Neymar afunguka suala la kuzomewa na mashabiki wa PSG | Muungwana BLOG

Neymar afunguka suala la kuzomewa na mashabiki wa PSG


Pamoja na Neymar kurejea katika kikosi cha timu yake ya PSG ikiwa nyumbani jana Parc des Princes katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Strasbourg, alikumbana na mtihani wa kuzomewa na mashabiki wa PSG.

Neymar amekumbana na wakati mgumu licha ya kupachika goli pekee la ushindi dakika za nyongeza na kuifanya PSG kushinda 1-0 katika mchezo huo, mashabiki wa PSG walikuwa wakimzomea mechi yote, hiyo inatokana na nyota huyo kulazimisha kuondoka katika majira ya usajili ya joto kurudi Barcelona kitu ambacho kilileta utofauti kati yake na uongozi.

"Sina cha kusema kwa mashabiki nawaelewa, najisikia huzuni, kuanzia sasa ninafahamu kila mechi nitakayocheza nitakuwa kama nacheza ugenini kwa upande wangu" Neymar alisema baada ya mchezo.

Aliendelea kwa kusema, "Kila mmoja anafahamu kuwa nilitaka kuondoka nilisema hivyo na nilirudia hivyo, sitaki kwenda ndani zaidi kwani ukurasa umefungwa, kwa sasa bado mimi ni mchezaji wa PSG na ninataka kujitoa zaidi uwanjani kwa ajili yao, niweke wazi sina tatizo na mashabiki wa PSG wala PSG kama klabu".