Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amezikaribisha Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini MwaAfrika (SADC) kutumia bandari ya Dar es Salaam mara baada ya ukarabati wake hasa gati namba sifuri kuanza kupokea mizigo.
Akizungmza Jijini Dar es Salaam alipotembelea kuona meli kubwa ya Mizigo yaMagari ya kampuni ya Meli ya Mv Grand Duke iliyotua bandarini jana , Waziri Kamwelwe amefurahishwa kuona meli hiyo kubwa yenye urefu wa mita 200 na uwezo wa kubeba magari 6,000 ambapo imetua ikiwa na magari 1,347 imedhihirisha uwezo wa bandari hiyo kwamba iko tayari kupokea mizigo mikubwa.

