Rais Magufuli, ameahidi kumlipia gharama za kwenda ‘Hijja’ Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga, Hamza Johari, kutokana na Uchapakazi mahiri aliouonyesha katika nafasi hiyo. Aidha Rais Magufuli amesema angekuwa na Binti yake angemuozesha Johari ili awe Mkwe wake.
Rais Magufuli amesema katika mwaka wa fedha uliopita, Mamlaka hiyo ilikusanya mapato ya Bilioni 71 kutoka Bilioni 40, na kwamba mwaka ujao wa fedha wanatarajiwa kukusanya kiasi cha shilingi Bilioni 82.

