Rais Dkt. John Magufuli anazindua Rada mbili za kuongozea ndege za uwanja wa ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere na uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro KIA.
Katika ufunguzi huo amewapongeza Watanzania wote kutekeleza mradi huu kwa sababu walilipa kodi na kama wasingelipa kodi mradi huu usingekuwepo.
"Leo hii tunakutana kuzindua rada hii kwakweli nimefurahi sana. Mimi sipendi miradi inayoishia njiani hasa niliyoweka jiwe la msingi mimi, ndio maana nimefurahi sana. Nakupongeza Mkurugenzi wa TCAA sina cha kukulipa ila ukitaka kwenda Hijja mimi nitalipia" amesema.
Ameendelea kwa kusema, " Yaliwahi kutengwa mabilioni ya fedha kwa ajili ya kununua rada lakini haikununuliwa. Ilikuwa inunuliwe moja lakini haikununuliwa. Aliyehusika kule Uingereza alijiuzulu lakini huku kwetu sijui kama walijiuzulu, yawezekana ndio wakosoaji wakubwa".
