Ufaransa yalaani mashambulizi ya Saudi Arabia


Ufaransa imelaani vikali mashambulizi ya ndege zisizo na rubani yaliyofanywa jana katika vituo vya mafuta vya Saudi Arabia.

Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa, imesema kuwa mashambulizi hayo yaliyotokea kwenye vituo vya mafuta vya Abqaiq na Khurais yameathiri kwa kiasi kikubwa uuzaji wa mafuta duniani na kwamba Ufaransa inasimama na kuonesha mshikamano kamili pamoja na Saudi Arabia.

Mashambulizi hayo yametajwa kuwa yanaweza kuongeza wasiwasi katika ukanda huo na kusababisha hali ya hatari ya kuzuka kwa mzozo. Aidha, Ufaransa imewataka washambuliaji kusitisha mashambulizi ya aina hiyo
Mpya zaidi Nzee zaidi