Yanga yaiadhibu Toto Africans bila huruma

Klabu ya Yanga imekamilisha mechi zake za kujipima nguvu katika kambi yake ya Mwanza kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Toto Africans jioni ya leo Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza.

Ushindi huo umetokana na mabao ya mshambuliaji mpya, David Molinga ‘Falcao’ aliyefunga mawili dakika ya 37 na 41 na kiungo mpya pia, Mzanzibari Abdulaziz ‘Bui’ Makame dakika ya 51.

Na ushindi huo unafuatia sare ya 1-1 kwenye mchezo uliopita dhidi ya timu nyingine ya Daraja la Kwanza, Pamba SC Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, bao la Yanga likifungwa na Molinga pia.

Baada ya mchezo huo, Yanga SC wanatarajiwa kupanda ndege kurejea Dar es Salaam tayari kuwakabili Zesco United Jumamosi wiki hii Uwanja wa Taifa katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mwisho ya kuwania kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items