Agizo la Rais Magufuli kwa Bibi Kikongwe wa Miaka 94 alieporwa Shamba na Kijiji,Latekelezwa

Agizo la Mh.Rais Dk. John Magufuli  alilolitoa kwa mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti la  kufuatilia Bibi Martha Kuzilwa (94 ) mkazi wa kijiji cha Loisinyai kata ya Oljoro namba 5  la kurejeshewa akari zake 300 alizoporwa na Serikali ya Kijiji limetekelezwa jana Jumamosi oktoba 12.2019 na Mkuu wa wilaya ya Simanjiro, Mhandisi Zephania Chaula, akiwa na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Yefred Myenzi kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo Mnyeti.