Loading...

10/07/2019

Bonanza la michezo kufanyika kila baada ya miezi miwili


Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw.Yusuph Singo amesema kuwa Bonanza la Michezo litaendelea kufanyika kila baada ya miezi miwili  na litahusisha michezo mbalimbali.


Bw. Singo ameyasema hayo Jijini Dodoma alipozungumza wakati akishukuru Watumishi wa Serikali na wananchi wa Jijini la Dodoma waliojitokeza kushiriki Bonanza hilo.

“Bonanza hili litafanyika kila baada ya miezi miwili lengo ikiwa ni kuimarisha afya zetu pamoja na kuimarisha upendo,amani na mshikamano tulionao Tanzania”alisema Bw.Singo.

Aidha Bw.Singo amesema kuwa Bonanza hilo litashirikisha michezo mbalimbali ikiwemo  mbio za taratibu,mazoezi ya viungo, mpira wa miguu,mpira wa pete,kuvuta kamba na michezo mingine.

Naye Afisa Habari Idara ya Habari Maelezo Bw.Daudi Manongi amesema kuwa Bonanza hilo limekuwa na faida nyingi kwani  limewakutunisha Watumishi wa Serikali na Wananchi wa Jiji la Dodoma katika kuimarisha afya zao na kubadilishana uzoefu katika kutekeleza kazi zao.

Katika bonanza hilo timu ya kuvuta kamba ya Wizara ya habari,Elimu na timu ya Joggin kutoka Dodoma ziliibuka washindi ,huku timu ya mpira wa miguu ya Serikali ikiifunga magoli matatu timu ya Boabao Queens ya Jiji la Dodoma iliyoambulia goli moja.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger