Dodoma FC yailaza Ihefu FC ligi daraja la kwanza



Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.

Baada ya kupoteza mchezo wao ugenini dhidi ya Boma FC, leo timu timu ya Dodoma FC imefanikiwa kuondoka na pointi zote tatu baada ya kuifunga timu ya Ihefu FC kwa bao moja kwa bila katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Bao pekee la Dodoma FC limefungwa kipindi cha kwanza na Rajabu Seif, kwa mpira wa adhabu ndogo nje kidogo ya eneo la hatari, na kuiweka timu yake mbele kwa bao hilo moja.

Kipindi Cha pili kilianza kwa kasi kubwa huku kila timu ikifanya mabadiliko kupata bao lakini hakuna timu iliyofanikiwa kupata bao, hadi mwisho wa mchezo Dodoma FC 1 na Ihefu FC 0.


Mpaka sasa Dodoma FC inapointi tisa 9 baada ya kushinda mechi tatu dhidi ya Cosmopolitan, Friends Rangers na Ihefu FC, na kupoteza mechi moja dhidi ya Boma FC Jijini Mbeya, mara baada ya mchezo huo kumalizika kocha wa Dodoma FC Mbwana Makata amesema timu yake inazidi kuimarika siku baada ya siku.

Amebainisha kuwa kwa sasa amewekeza nguvu nyingi kuhakikisha timu yake inapata magori mengi hasa katika michezo yake ya nyumbani, ameomba mashabiki waendelee kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao.

" Timu yangu naona inazidi kuimarika siku baada ya siku kilichobaki ni kuelekeza nguvu nyingi katika eneo la ushambuliaji ili waweze kupata magori mengi hasa katika mechi za nyumbani" amesema Makata.

Nae kocha wa Ihefu FC ambaye ni mchezaji wa zamani wa Tukuyu Stars na Mtibwa Sugar, Salhina Mjengwa, amesema timu yake imecheza vizuri ila makosa madogo madogo ndio yamepelekea kupoteza mchezo huo na sio kwamba walizidiwa na timu pinzani.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia