Kenya: DT Dobie yazindua Mercedes Benz


Kampuni ya magari ya DT Dobie imezindua gari mpya aina ya Mercedes Benz yenye injini ya ukubwa wa cc 1500.

DT Dobie imesema gari hilo aina ya 180-Class ltakuwa na utendaji mzuri na pia gharama nafuu ya matumizi yake ya mafuta.

Mkurungezi wa DT Dobie nchini Kenya Ian Middleton amesema bei ya gari hilo jipya pia itakuwa nafuu ili kuwezesha Wakenya wengi wa tabaka la wastani kulimudu.