NMB Yachangia Milioni 105 kwenye sekta ya elimu Arusha



Na Sechelela Kongola,Arusha.

Benki ya NMB imechangia kiasi cha shilingi milioni 105  kwenye sekta ya elimu mkoani Arusha kwa kutoa madawati na kuchangia vifaa vya ujenzi katika shule mbalimbali za msingi na sekondari lengo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kutoa huduma ya elimu bure kwa watanzania wote.

Wakikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha aliyepokea ,amesema kuwa benki hiyo imekua mfano wa kuigwa kwa kutoa sehemu ya faida wanayoipata katika kuihudumia jamii inayowazunguka ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto zilizoko kwenye jamii.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema kuwa msaada huo utatumika vizuri na kusaidia kuinua kiwango cha ufaulu wa wanafunzi kwa kuboresha miundombinu ya elimu.

Afisa Mkuu wa Huduma Shirikishi benki ya NMB Nenyuata Ole  Mijooli amesema kuwa msaada huo ni muendelezo wa benki hiyo kutoa sehemu ya faida wanayoipata na kuirudisha katika jamii ili iweze kuwasaidia hususan katika sekta ya elimu ambayo ni kichochea cha maendeleo ya taifa.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Mringa pamoja na Mwanafunzi wa shule hiyo Salim Magaka na Angle Mathias ambaye ni Mwanafunzi shule ya Sekondari Mringa wameipongeza benki ya CRDB Kwa kutoa madawati pamoja na mabati ya kupaua madarasa na mabweni katika shule hiyo hali itakayopunguza uhaba wa madarasa na kuinua kiwango cha ufaulu.