Na. Baraka Messa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ameita Wizara ya Ujenzi na Tanroads kuhakikisha barabara ya Mpemba Ileje inayojengwa kwa kiwango cha rami kuhakikisha inakamilika ifikapo mwakani 2020 mwez septemba.
Dkt. Magufuli amezungumza hayo akiwa ziarani mkoani Songwe baada ya kuzindua barabara hiyo na kuweka jiwe la Msingi katika mji mdogo wa Mpemba.
Alisema barabara hiyo yenye urefu wa kilomita hamsini ujenzi wake ulianza mwaka 2017 ambapo ilitakiwa ukamilike mwezi agost mwaka huu lakin cha kushangaza mpaka sasa ni mwezi October mradi bado kabisa kukamilika.
Dkt Magufuli alisema mkandarasi huyo anachelewesha mradi ambao ni muhimu kwa wananchi wa ileje , Tunduma na wanasongwe kwa ujumla .
"Mradi huu una gharama ya shilingi billion 109 ambazo ni pesa nyingi sana , hizi ni kodi za wananchi ambazo zimekaa kwa muda wa miaka mitatu pasipo kutumika vizur
Mradi unatumia fedha nyingi ambapo kilomita moja sawa na na shilingi bilioni mbili, hii ni gharama kubwa sana" alisema Rais
Dkt Magufuli alisema mradi huo wa barabara wenye kilomita zaidi ya 50 unasimamiwa na serikali kwa asilimia 100 kwa fedha za serikal na kuchelewa kukamilika ni kuchelewesha na kukwamisha fedha za wananchi.
Aliwataka Tanroad na wizara ya ujenzi kumsimamia mkandaras huyo anayesimamia Barbara huyo , na kuwataka kumsimamisha kazi ikiwa atashindwa kwendana na kasi ambayo serikali inauhitaji.
Aidha Dkt Magufuli alizindua hospitali ya mji wa Tunduma inayojengwa kwa gharama ya zaid bilion 4 ambapo ameahid kutoa billion 2.4 ilikukamilisha hospital hiyo zilizoombwa na mkuu wa mkoa wa Songwe Brigedia General Nicodemas Mwangela ili kukamilisha ujenzi ambao unategemewa kuhudumia wananchi wengi wa Tunduma na nchi jiran
Izack wazir wa ujenzi alisema kuwa bara bara hiyo itakamilika mwakani Septemba , na kukamilika kwake kutaimalisha mahusiano na mawasiliano kati ya Tanzania na nchi jirani ya Malawi na kuinua uchumi has a biashara.
