Rais wa baraza la Ulaya ambwatukia waziri mkuu wa Uingereza kuhusu Brexit

Rais wa baraza la Ulaya Donald Tusk amemueleza kwa hasira waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson kwamba Brexit sio mchezo wa kijinga wa kulaumiana na kumtaka moja kwa moja kueleza wapi anapotaka kuyafikisha mazungumzo hayo yanayosambaratika kwa kasi.

Baada ya ofisi ya waziri mkuu Johnson kutoa majibu mabaya kuhusu mawasiliano ya simu kati ya waziri mkuu huyo na kansela wa Ujerumani Angela Merkel, Tusk mara moja alijibu kupitia twitter kwamba mazungumzo ya Uingereza na Umoja wa Ulaya hayamaanishi kutupiana lawama, iwapo Brexit itafikiwa bila makubaliano.

Msemaji wa tume ya Ulaya Mina Andreeva hata hivyo amesisitiza kwamba nafasi ya Ulaya kuhusu mazungumzo hayo haijabadilika na kuongeza kuwa mazungumzo ya kiufundi yanaendelea.

Ofisi ya Johnson iliarifu kuwa kansela Merkel amesema anaamini makubaliano ya Brexit kwa kiasi kikubwa hayatafikiwa baada ya mazungumzo hayo ya simu.