Rais wa Cameroon Paul Biya ameamuru kuachiliwa huru kwa watu zaidi ya 300 waliokamatwa kwa makosa madogo kuhusiana na vurugu za upande wa wanaozungumza Kingereza Magharibi mwa nchi hiyo.
Koloni hilo la zamani la Ufaransa la Afrika Magharibi limetumbukia katika vurugu tangu maeneo yake mawili makuu yanayozungumza Kiingereza, Kaskazini-Magharibi na Kusini-Magharibi, kutangaza mwaka 2016 kuwa wanataka kujitenga na kuunda nchi yao mpya itakayopewa jina la Ambazonia.
Agizo hilo, lililosainiwa na katibu mkuu wa rais, Ferdinand Ngoh Ngoh, lilitolewa wakati wa mazungumzo yaliyoitishwa na Biya kumaliza mapigano kati ya wanaotaka kujitenga na wanajeshi.
