Rwanda: Mhubiri aliyewakashifu vibaya wanawake afukuzwa


Mhubiri na mmiliki wa kituo cha redio cha Amazing Grace, raia wa Marekani Gregg Schoof aliyekamatwa mapema wiki hii jijini Kigali nchini Rwanda amefukuzwa nchini humo

Schoof amekuwa nchini Rwanda tangu mwaka 2003, kuhubiri lakini mwaka uliopita, kituo chake cha redio kilifungwa baada ya kuhubiri kupitia redio yake kuwa, wanawake ni malaya na ibilisi.

Alikamatwa siku ya Jumatatu, akiwa na mwanaye wakati alipokuwa anataka kuwahotubia wanahabari jijini Kigali akilenga kuishtumu seirkali ya Rwanda.

Idara ya uhamiaji inasema, mtoto wake ambaye hakutajwa jina aliachiliwa huru lakini, baba yake amefukuzwa kwa sababu mbili, kwanza, kibali chake cha kufanya kazi kilikuwa kimeisha lakini pia hakuwa na sababu ya kuwa Rwanda kwa sababu kituo chake cha redio kilishafungwa.

Kanisa la Mhubiri huyo ni miongoni mwa Makanisa 700 yaliyofungwa mwezi Februari, baada ya kushindwa kutimiza masharti ya serikali kuhusu kufungua kanisa.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items