Upangaji Nyanda za malisho wasaidia kupunguza vifo vya Mifugo


Na. Ferdinand Shayo, Manyara 

Upangaji wa nyanda za malisho kwa kufuata misimu ya kiangazi na masika umesaidia kupunguza vifo vya mifugo inayokufa kwa kukosa  malisho hususan katika Wilaya za wafugaji za Simanjiro, Monduli na Ngorongoro kutokana na vijiji kuanza kujiwekea akiba ya malisho wanayoitumia hasa katika kipindi kiangazi kikali hivyo kunusuru mifugo yao

Hayo yameelezwa Mkurugenzi wa shirika la Ujamaa Community resource team (UCRT) Makko Sinandei katika kikao maalumu cha namna ya kupanga na kusimamia nyanda za malisho ambapo vijiji zaidi ya 100 katika wilaya hizo tatu  vimepatiwa mafunzo na kutenga hekta milioni 1 kwa ajili ya malisho ambazo zimesaidia kunusuru mifugo kwani mwaka 2009 zaidi ya asilimia 25 ya mifugo ya wilaya ya Longido iliangamia kwa kukosa malisho.

Afisa Mifugo wa kata ya Terrat  Petro Lukumay mesema kuwa kipindi cha nyuma mifugo mingi iliangamia kwa kukosa malisho lakini kwa miaka ya hivi karibuni hakuna mifugo iliyokufa kutokana na juhudi za UCRT kwa kushirikiana na halmashauri na vijiji wameweza kutenga malisho na akiba za malisho hivyo imesaidia hata kupunguza migogoro ya wafugaji na wakulima.

Kaimu Mkurugenzi idara ya uendelezaji wa malisho na vyakula vya mifugo Asimwe rwiguza ameipongeza shirika la UCRT kwa kuiwezesha jamii kutenga nyanda za malisho pamoja na  kuwaonya  viongozi Wanaobadilisha kinyamela matumizi ya nyanda za malisho kuwa maeneo ya makazi bila kufuata utaratibu wa kisheria watachukuliwa hatua Kali ili kulinda nyanda za malisho.

Kwa upande wao wafugaji Lotolie Losinde  na Godson Nduya ambaye ni Mwenyekiti wa kijiji cha Terrat wamesema kuwa licha ya juhudi zinazofanywa za kutenga malisho bado kuna baadhi ya viongozi ambao wamekua wakibadili matumizi ya ardhi ya malisho na kugawa viwanja kwa ajili ya makazi suala ambalo limekua likiathiri ufugaji huku Viongozi wa vijiji wakikiri kuwepo kwa changamoto hiyo
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia