Wafugaji wamuomba Waziri wa Maliasili aongeze muda wa Tume ya Ardhi mseto



Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Wafugaji wanaoishi katika eneo la mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro iliyoko wilayani Ngorongoro mkoani Arusha wamemuomba Waziri wa maliasili Hamis Kigwangala kuongeza muda kwa tume ya mapitio ya ardhi mseto kukusanya maoni ya wananchi kwani muda wa siku 6 hautatosha kupata maoni ya wenyeji kutokana na ukumbwa wa eneo husika.

Akizungumza na wanahabari Mwenyekiti wa Baraza la Wafugaji Ngorongoro Edward Maura  amesema kuwa licha ya Waziri Kigwangala kusikia kilio cha wafugaji na kuongeza idadi ya wafugaji kuwa wawakilishi katika tume hiyo ya ardhi mseto bado muda wa kukusanya maoni ya wananchi umekua ni mdogo kiasi cha siku 6 pekee ambazoo zinaweza kuathiri ufanisi wa kazi hiyo unaweza kupungua.

Mwenyekiti huyo ameitaka Mamalaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kutokufanya maamuzi yoyote ambayo yataathiri kazi ya tume hiyo kwani bado tume hiyo haijamaliza kazi yake na kuja na majibu .

Katibu wa Baraza hilo Johanes Tiamasi amesema kuwa baraza hilo ni sauti ya wafugaji hivyo halitachoka kuwatetea wafugaji na kusisitiza kuwa wataendelea kujenga mahusiani bora na mammala ya hifadhi ili kuchcochea utalii endelevu.

Mjumbe wa Baraza hilo Lazaro Saitoti amesema kuwa mapendekezo ya ugawaji wa eneo ya ngorongoro kama nyanda utaathiri ustawi wa jamii,na ufugaji kwa ujumla kwani wafugaji wana mchango mkubwa katika uhifadhi
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia