Wahamiaji 13 wafariki kufuatia kuzama kwa mashua

Mashua iliyobeba karibu wahamiaji 50 ikitokea Tunisia yazama baharini karibu na visiwa vya Lampedusa mashariki mwa Italia. Miili 13 yapatikana huku watu 22 wakiokolewa.

Shirika la habari la Italia Ansa, limeripoti kwamba watu wote miongoni mwa waliopoteza maisha ni wanawake.

Kwa mujibu wa habari iliyotolewa na BBC kituruki, miongoni mwa waliopoteza maisha ni watoto 8.

Taarifa iliyotolewa na vikosi vya usalama wa pwani nchini Italia inasema Jumapili usiku walipata taarifa ya kuwapo kwa mashua iliyobeba karibu wahamiaji 50 katika mwambao wa Lampedusa.

Baada ya taarifa hiyo wakiambatana na polisi kwa kutumia boti mbili walikwenda kuwachukua wahamiaji hao katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hali mbaya ya hewa na bahari na kusogea ghafla kwa wahamiaji hao, mashua hiyo ilibinuka na kuzama.

Baada ya juhudi za utafutaji na uokoaji miili 13 ilipatikana na watu 22 waliokolewa.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items