Wanafunzi wakamatwa na Polisi kwa tuhuma za kumuua mwenzao


Jeshi la polisi  Kahama mkoani Shinyanga linawashikilia wanafunzi nane wa shule ya sekondari seeke kwa tuhuma ya kumshambulia na kumjeruhi Costantine Makoye mwanafunzi mwenzao majeraha ambayo yamesababisha kufariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Halmashauri ya Mji Kahama.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard, Abwao amethibitisha kushikiliwa kwa wanafunzi hao na kusema kuwa tukio hilo limetokea septemba mwaka katika kanisa la SDA Wasabato Kahama kulikuwa na sherehe ya kuwaaga wanafunzi washirika wa kanisa la SDA wanaotarajia kuhitimu kidato cha Nne.

Amesema Baada ya sherehe kuisha katika kanisa hilo wakati wanafunzi wanatawanyika alitokea Constantine Makoye akiwa na vijana wenzie wapatao 10 ambao hawajafahamika mara moja na haijulikani kama ni walikuwa ni miongoni mwa waalikwa katika sherehe hiyo.

Kamanda Abwao amesema wanafunzi hao walimvamia mwanafunzi aitwaye Isaya Athuman (18) mwanafunzi kidato cha nne seeke secondary, na kutaka kumnyang'anya viatu alivyokuwa amevaa na wengine waliwanyang'anya maji ya kunywa wanafunzi waliokuwa katika sherehe hiyo.

Ndipo wanafunzi hao walipopiga kelele na yowe kwamba wamevamiwa, waliungana pamoja na kuanza kuwarushia mawe hao waliovamia sherehe hiyo na Wavamizi hao walikimbia na kutawanyika lakini Constantine Makoye alizidiwa na kulala chini na wanafunzi hao walimtelekeza hapo.

Amefafanua kuwa Baadae aliamka na kwenda nyumbani kumjulisha Babu yake ambaye alimpeleka kutibiwa katika hospitali ya serikali Kahama bila kutoa Taarifa kituoni hadi alipozidiwa tarehe 01/10/2019 akiwa hawezi kuongea ndipo ndugu walijulisha kituoni na jalada lilifunguliwa kwa kosa la kujeruhi na maelekezo ya mwanafunzi huyo hayakupatikana kutokana na hali yake kuwa mbaya.


Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items