Takriban watu 25 wamefariki na wengine wengi hawajulikani walipo baada ya kimbunga Hagibis kuikumba Japan.
Haya ni kulingana na maafisa wakuu wa nchi hiyo waliosema hayo hii leo huku waokoaji wakijitahidi kuwaokoa watu waliokwama kutokana na janga hilo la mafuriko.
Dhoruba hiyo ya mvua ambayo haijawahi kushuhudiwa imesababisha maporomoko hatari ya ardhi na mito kufurika.
Hadi leo asubuhi, dhoruba hiyo iliyopungua makali ilikuwa imegeuza njia na kuelekea baharini lakini mafuriko makali yameripotiwa katika maeneo kadhaa ikiwa ni pamoja na eneo la Kati mwa Japan la Nagano ambako daraja la mto Chikuma lilivunjika na kusababisha maji kuenea katika maeneo jirani na kujaa hadi ghorofa ya pili ya nyumba.Jeshi la Japan limepeleka wanajeshi elfu 27 kusaidia katika oparesheni hizo.