Loading...

11/10/2019

CCM yapita bila kupingwa katika vijiji 6,248 kati ya 12,319


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo, amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) kimepita bila kupingwa katika vijiji 6,248 kati ya 12,319 mitaa 1,169 kati ya 4,263 na vitongoji 37,505 kati ya 64,384.

Waziri Jafo ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, kuhusiana na mwenendo wa Uchaguzi huo.

Amesema kati ya wagombea waliochukua Fomu wagombea 41,2872 sawa na asilimia 74 wakiwa ni wa CCM, Wagombea 105,937 sawa na asilimia 19 ni CHADEMA, Wagombea 24,592 sawa na asilimia 4 wakiwa ni CUF na wagombea 8,526 Sawa na asilimia 1.5 wakiwa ni wa ACT huku vyama vingine vikiwa na asilimia 0.1 ya wagombea.

Katika hatua nyingi Waziri Jafo amesema Mamlaka ya Uchaguzi inawatambua wagombea wa vyama vya upinzani vilivyotangaza kujitoa kwenye Uchaguzi huo.

.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger