China yakanusha kuingilia siasa za Australia

China leo imekanusha madai ya kuingilia siasa za Australia ikisema haijawahi kujaribu kuingilia masuala ya ndani ya mataifa mengine na kusisitiza haina mipango ya kufanya hivyo.

Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya China, Geng Shuang amewaambia waandishi habari mjini Beijing, kuwa vyombo vya habari nchini Australia vimetunga madai hayo ya uingialiaji.

Siku ya Jumapili kipindi kimoja cha televisheni na magazeti kadhaa nchini Australia yaliliripoti kuwa mtandao wa kijasusi wa China ulimlipa fedha mfanyabiashara mashuhuri wa magari mjini Melbourne ili awanie kiti katika bunge la Australia.

Mamlaka za usalama na ujasusi za Australia zimesema tayari zinachunguza madai ya mpango wa China wa kuingiza wakala wake wa ujasusi ndani ya bunge la nchi hiyo.

Mpya zaidi Nzee zaidi